1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pistorius apoteza katika kesi ya rufaa

13 Machi 2015

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amepoteza kesi ya rufaa kuhusu hatua ya mahakama ya kumuondolea mashtaka ya mauaji ya mchumbake wake Reeva Steenkamp

https://p.dw.com/p/1Eqf8
Oscar Pistorius Gerichtssaal Pretoria
Picha: Reuters/A. Skuy

Mawakili wa Oscar Pistorius wameshindwa katika juhudi za kuwazuia waendesha mashtaka dhidi ya rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa kwa mwanariadha huyo mlemavu wa Afrika KUSINI ya kuua bila kukusudia na kutaka tena hukumu ya mauaji dhidi yake kwa kumpiga risasi mchumba wake Reeva Steenkamp.

Jaji Thokozile Masipa ametoa uamuzi katika mahakama ya Johannesburg kwamba ombi hilo likataliwe. ''kwa maoni yangu, iwapo nitaliruhusu ombi hilo nitakuwa nautathmini upya uamuzi wangu'', na nadhani kuwa, kimchakato, itakuwa vibaya kukubali au kukataa ombi hili. Kwa hiyo, amri ninayotoa kuhusu suala hili ni kulitupilia mbali ombi hilo.

Pistorius alimpiga risasi na kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp mnamo mwezi Februari 2013. Alipewa hukumu ya miaka 5 jela kwa mashtaka ya mauaji ya kutokusudia. Mwanariadha huyo aliye na ulemavu wa miguu yote miwili aliondolewa mashtaka yote mawili ya mauaji ya kukusudia.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri:Gakuba Daniel