1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Picha mpya zaonesha Bi Bhutto akipigwa risasi

30 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Ci38

ISLAMABAD.Siku tatu baada ya kuawa kwa Bi Benazir Bhutto, kituo kimoja cha televisheni cha Pakistan kimetoa picha zinazomuonesha mtu mwenye silaha akimfyatulia risasi bi Bhutto kabla ya mlipuko kutokea.

Picha hizo iwapo zitathbitika kuwa kweli, zitapingana na zile zilizotolewa na serikali ya kwamba alijigonga kichwa kwenye paa la gari yake baada ya kurushwa na mlipuko wa bomu.

Serikali ya Rais Pervez Musharraf inalituhumu kundi la kigaidi la al Qaida kuhusika na shambulizi la bomu hilo.

Chama cha Bi Bhutto kinaituhumu serikali hiyo ya Pakistan kuhusika na mauaji hayo, ambapo Marekani mshirika mkubwa wa Rais Musharaff imetaka kufanyika uchunguzi wa kina kuhusiana na mauaji hayo.

Wakati huo huo maelfu ya waombelezaji wamekusanyika katika mji wa nyumbani kwa Bi Bhutto wakiishutumu serikali ya Paksitan kwa mauaji ya kiongozi wao.

Chama cha PPP kinakutana hii leo kumchagua mrithi wa bi Bhutto na pia kuamua iwapo kiususie uchaguzi mkuu wa tarehe nane mwezi ujayo.