Picha hutengeneza siasa: Vipi Kohl alijinadi
3 Julai 2017DW : Klaus Honnef,tafadhali tueleze wakati ulipomuona Kohl ?
Klaus Honnef : Nilikutana naye wakati mimi na mke wangu tulipoalikwa kwenye maonyesho ya sanaa katika Ofisi ya Kansela mwaliko uliotolewa na kansela wa zamani Helmut Schmidt.Alijitokeza baadae akishuka ngazi.Mara nilipomuona utani wote juu ya Kohl niliokuwa nao mawazoni ulikufa kwani kamwe sikuwahi kumwazia yeye akiwa kama kundi la barafu likitembea Sikumwazia kwamba alikuwa ni mtu wa umbo kubwa kama vile alivyo hasa.
Iwapo unazichambuwa picha za Kohl ipi inayotowa mwangwi zaidi ?
Nyingi ya taswira ambazo zimezama katika kumbukumbu zangu zinaonyesha umbo ambalo nimeliona mwenyewe.Ubaridi wake lakini pia uwezo wake wa kumchunguza mtu kwa kumuangalia machoni. Halikadhalika ubora wake mkubwa ambao angalau anaunururisha sio kwa kupitia mwili wake.
Tuchukulie picha mashuhuri ya Kohl na Mitterand (Rais wa Ufaransa)katika medani ya vita ya Verdun. Hii imepangwa?
Bila ya shaka imepangwa. Nina imani kwamba takriban picha zote za wanasiasa hivi leo huwa zimepangwa. Na picha hii mashuhuri haitokani na mawazo ya Helmut Kohl bali ni Mitterand ambaye alikuwa hodari kwa jinsi anavyotaka jicho la umma limuangalie kwa mtizamo gani. Helmut Kohl pia alikuwa hodari kuigiza. Tokea enzi za Willy Brandt wanasiasa wamejifunza namna ya kutembea wakati kamera zinapowamurika.Wameendeleza ubora wa viwango ambao waigizaji wakuu wa sinema wamekuwa nao.
Katika picha ya kupendeza ya Kohl na mke wake Hannelore na watoto wake wawili wa kiume kansela huyo alifanikiwa kuelezea maadili yake ya kisiasa?
Kabisa.Kama vile tunavyojuwa hivi sasa furaha yake haikuishia tu kama picha hii inayoashiria. Lakini kila taswira inayosambaa miongoni mwa wananchi ndivyo inavyomuweka mtu kuwa alama fulani ya madaraka.
Picha hutengeneza siasa ...mara nyingi kuliko hata maamuzi. Picha hiyo yenye kuonyesha familia furahani,mtu mzuri wa familia inakwenda sambamba na taswira ya madaraka katika picha nyengine nyingi za Helmut Kohl. Hii ni sehemu ya picha kwa jumla. Hutaki kuwa mwanasiasa mwenye nguvu asiependa maingiliano.Anapaswa aonyeshe ubinaadamu fulani na uchangamfu wa mtu wa familia.
Kuna picha nyingi za Kohl idadi isiohesabika.Alikuwa akitaka aonekane vipi?
Daima kama mwanasiasa mwenye mafanikio kwangu mimi mojawapo ya picha nzuri ni iliopigwa na Helmut Newton katika bustani ya makao ya Kansela mjini Bonn. Helmut Kohl alikuwa mbele ya mti wa mwaloni.Hii ni picha yenye kuashiria maelewano baina ya pande mbili.Macho ya mpiga picha yalitazamana na yale ya Kansela.Hii ilikuwa ni picha ya taifa. Lakini ni picha ya usanii kwa sababu haifai kwa mahala rasmi.
Unaweza kusema Kohl alikuwa bingwa wa utayarishaji kwa vyombo vya habari ambaye kwa ustadi alitumia kwa faida yake taswira yake mwenyewe binafsi?
Ndio kwa uhakika kabisa.
Ungeliweza kusema ibada za mazishi : Hafla ya kitaifa ya Ulaya huko Srasbourg , kusafirishwa kwa mabaki yake kwa meli mto Rhine,misa katika kijiji chake cha Speyer.Yote hayo yanaoana pia kwenye picha?Kohl angeliyapenda?
Kweli kabisa.Sikuwa hasa shabiki wa Kohl juu ya kwamba nahusudu mafanikio yake.Lakini ukweli kwamba taifa la Ujerumani linahangaishwa na haiba ya kansela huyu wa zamani na kwamba Rais wa serikali ya shirikisho ya Ujerumani hakuandaa tukio la kitaifa jambo hilo linanipa mashaka. Kwa sababu Helmut Kohl alikuwa kansela wa muungano na pia ni alama ya Ujerumani ambayo hivi sasa inakabiliwa na mabadiliko makubwa.Na hakuna ajuaye inaelekea wapi.Kwa hali hiyo tukio la kitaifa lingelileta taathira ya upatanishi. Na nina imani kwamba Kohl angelipenda sana.
Profesa Kalus Honnef aliyezaliwa mwaka 1939 anachukuliwa kuwa mmojawapo wa wahakiki wa sanaa na picha, mwanahistoria na msimamizi wa makumbusho nchini Ujerumani.Ni mwandishi mwenza wa "Art of the 20th Century" Sanaa ya Karne ya Ishirni.
Mwandishi : Stefan Dege/Mohamed Dahman
Mhariri : John Juma