1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PESA TU HAZITOLETA AMANI:

11 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFtA
ROMA: Mawaziri wa kigeni wa Israel na wa Wapalestina wametangaza juhudi mpya ya kuboresha ugawaji wa misaada ya kimataifa katika Ukingo wa magharibi na Ukanda wa Gaza.Silvan Shalom wa Israel na Nabil Shaath wa Wapalestina walikutana pembezoni mwa mkutano wa mwaka wa wafadhili wa Utawala wa ndani wa Wapalestina mjini Roma.Waziri wa kigeni wa Norway Jan Petersen amesema pesa peke yake hazitoleta amani katika eneo la Mashariki ya Kati.Katika mkutano huo wa wafadhili,lawama zaidi zilielekezwa upande wa Israel:hatua za kufunga vituo kwa sababu za usalama zimeumiza uchumi wa Wapalestina na kuzuia kazi za mashirika ya misaada,na pia mashambulio ya kijeshi dhidi ya wanamgambo yameteketeza miradi kadhaa ya wafadhili.Hata Wapalestina pia wamekosolewa kwa kushindwa kusitisha mashambulio dhidi ya Waisraeli.Kwa wakati huo huo Wapalestina wamehimizwa kuendelea na mageuzi kwenye idara za pesa na usalama.