Pengo kati ya mataifa tajiri na maskini latishia umaskini
18 Julai 2023Banga ameyasema hayo katika mkutano wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu kutoka mataifa ya kundi la G20, unaokamilika hii leo nchini India. Mataifa mengi bado yanaendelea kufufuka kutokana na athari za janga la UVIKO-19 na vita vya Urusi nchini Ukraine, ambavyo vilisababisha kupanda kwa gharama za mafuta na vyakula.
Uamuzi wa Urusi kujiondoa katika mkataba wa nafaka watishia mataifa maskini
Mazungumzo ya G20 yamekuja baada ya Urusi kukataa hapo jana Jumatatu, kurefusha makubaliano yanayoruhusu usafirishaji muhimu wa nafaka kutoka Ukraine kupitia bahari Nyeusi, na kuzusha hasira kutoka Umoja wa Mataifa, ambao umeonya kuwa mamilioni ya watu maskini duniani ndiyo watakaolipa gharama.Waziri wa fedha wa Afrika Kusini Enoch Gondo-ngwana ameonya kuwa uamuzi huo huenda ukaathiri bei za chakula, ambazo zitayagusa zaidi mataifa maskini.