Pendekezo la kuanzisha Wizara ya maendeleo ya dunia latolewa.
18 Oktoba 2013Mkuu huyo wa taasisi ya sera ya maendeleo Bwana Dirk Messner amesema badala yake nchi hizo masikini zinapaswa kushirikishwa katika kutatua matatizo ya dunia kama vile mabadiliko ya tabia nchi na migogoro ya kiuchumi.
Messner ameeleza kwamba asa unahitajika muundo mpya katika uhusiano baina ya nchi zinazoendelea na nchi za viwanda. Na kwa ajili hiyo amependekeza kuazishwa kwa wizara mpya nchini Ujerumani.
Wizara ya maendeleo ya dunia badala ya ile iliyopo sasa inayoitwa wizara ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo. Kulingana na muundo wa sasa wizara hiyo imekuwa inatoa misaada ya maendeleo ili kuyatatua matatizo katika nchi zinazoedndelea.
Lakini bwana Messner anataka wizara mpya iwe na jukumu la kuzishirikisha nchi zinazoendelea katika kuyatatua matatizo ya dunia. Katika kipindi cha miaka 50 ya sera ya maendeleo tulijenga taratibu na tuliweka njia maalumu-Lengo limekuwa kuzisaidia nchi zinazoendelea kuyatatua matatizo katika nchi hizo.
Hata hivyo hilo lipaswa kuendelea kuwa sehemu ya jukumu.Lakini yapo majukumu mengine muhimu.Tunachohitaji sasa ni taratibu na njia zitakazotuwezesha kuyatatua matatizo ya dunia pamoja na nchi zinazoendelea na nchi zinazoinukia kiuchumi.
Taratibu za za kuwa na sera mpya ya maendeleo zatolewa
Kwa mfano lazima tuyashughulikie masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na lazima tuyaimarishe masoko ya fedha ya kimataifa." Mkuu huyo wa taasisi ya sera ya maendeleo ya mjini Bonn bwana Messner amesema ruwaza ya hadi sasa, yaani ya misaada kutoka kwa matajiri kwenda kwa masikini haifai tena.Kinachohitajika sasa ni muundo mpya, sera mpya ya mandeleo.
"Zaidi ya hayo tunapendekeza kwamba wizara hiyo mpya ijikite katika mambo matatu tu na siyo katika masuala yote ya kimataifa. kwani kufanya hivyo kutakuwa ni kujitwika mzigo usiobebeka", Alisema bwana Messner.
"Jambo la kwanza linahusu mabadiliko ya tabia nchi sambamba na suala la nishati pili kusonga mbele katika ushirikiano wa sayansi na tekinolojia, na tatu ni kuendelea na harakati za kupambana na umasikini"
Jee upo uwezekano wakuundwa wizara hiyo mpya inayopendekezwa na mtaalamu huyo wa masuala ya maendeleo Dirk Messner ambae pia anaishauri serikali ya Ujerumani juu ya masuala ya maendeleo?
Bwana Messner amejibu kwa kusema kuwa anatumai itawezekana kuanzisha mjadala juu ya pendekezo lake.Lakini itakuwa muhimu ikiwa Kansela wa Ujerumani ataliona pendekezo hilo kuwa lina maana.
Mwandishi:Wißing,Carolyn
Tafsiri:Mtullya Abdu
Mhariri: Bruce Amani