Pemba: Mvutano kati ya KMKM na watetezi wa haki
28 Juni 2016Matangazo
Tukio hilo lilitokea wakati wananchi kadhaa wakishikiliwa kwa tuhuma za kujihusisha na uharibifu wa mashamba na mali mbalimbali za makada wa Chama cha Mapinduzi kisiwani Pemba. Kutaka kufahamu zaidi kuhusu kinachoendelea Josephat Charo amezungumza na Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu wa chama cha Wananchi, CUF, Pemba, Mwinyi Juma.