1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Passpoti zenye data zote za mhusika zitaanza kutumika nchini Ujerumani mwezi November ujao

2 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF7f

Berlin:

Kuanzia november mosi ijayo,wajerumani wataanza kutumia passpoti zenye alama juu ya hali ya maisha ya mhusika.Habari hizo zimetangazwa na waziri wa mambo ya ndani Otto Schilly.Mwanzoni passpoti hizo zitakua na chembe inayoonyesha picha ya mhusika,na kuanzia mwaka 2007,zitaingizwa pia alama za kidole.Waziri wa mambo ya ndani Otto Schilly amesema utaratibu wa kunasa maelezo juu ya hali na maisha ya mhusika ndani ya passpoti utafanya iwe shida kabisa kutengeneza passpoti za udanganyifu ,au isiwezekane kabisa.Wataalam lakini wa hifadhi ya data wanakosoa utaratibu huo.