Park atoka Ikulu na kuhamia mahabusu
31 Machi 2017Rais huyo wa zamani wa Korea Kusini aliingia kituo cha rumande cha Seoul na gari ndogo nyeusi kabla ya alfajiri siku ya Ijumaa baada ya mahakama kutoa uamuzi akamatwe kwa tuhuma za rushwa .
Park alijiandikisha rumande kwa kuisajili kadi yake ya makaazi, kufanya uchunguzi wa afya, na kukabidhi vitu vya binafsi ikiwemo pini ya nywele iliyoandikwa jina lake. Baada ya hayo, alivaa sare za rumande zenye rangi ya kijani na kufungiwa katika chumba chake, alisema mfanya kazi mmoja wa rumande hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake. Chumba chake cha rumande kina televisheni, choo kidogo, meza na godoro. Park anatakiwa kuamka saa kumi na mbili asubuhi kila siku na lazima alala saa mbili usiku.Pia atakula katika chumba hicho kama wafugwa wengine na analazimika sahani yake mwenyewe, alisema mfanyakazi mmoja.
"Atafanya yale yote yanayofanywa na wafungwa wengine," alisema afisa mmoja wa rumande hiyo. Park anatarajiwa kuwepo katika rumande hiyo kwa miezi kadhaa huku kesi yake ikiendelea kuskilizwa mahakamani.
Historia fupi ya Park Guen-hye
Aliwahi kukaa katika Ikulu ya Korea ya Kusini mara mbili. Mara ya kwanza alikaa kama mtoto wa kiongozi wa kijeshi Park Chung -hee, ambaye alihamia katika nyumba hiyo ya ikulu ya Blue House 1963, miaka miwili baada ya kuipindua serikali na kuchukua madaraka.
Kiongozi huyo wa zamani alitoka katika nyumba hiyo baada baba yake kuuwawa 1973 lakini baada ya kushinda uchaguzi wa desemba 2012 alirejea tena kukaa katika ikulu.
Rais huyo wa zamani alitakiwa kumaliza muhula wake wa urais Februari 2018 lakini aliondolewa madarakani baada ya kukutwa na hatia ya rushwa. Park ni rais wa pili wa nchi hiyo kuwa rumande mjini Seoul. Roh Tae Woo ambaye alikuwa rais kuanzia 1988 mpaka 1993 pia aliwahi kutumikia kifunga 1995 .pia kwa makosa ya rushwa.
Waziri wa kilimo chini ya uongozi wa Park Cho Yoonsun na mkuu wa zamani wa wafanyakazi, Kim Ki-choon, pia wako katika rumande hiyo hiyo. Kituo cha mahabusu aliko Park mjini Soul, kilifunguliwa 1987, kimechukua mahala pa gereza lililojengwa 1908. Wakati wa utawala wa kikoloni wa kijapani nchi Korea ya Kusini, sehemu hiyo ilikuwa ikitumiwa kwa kuwatesa wanaharakati wa wakupigania uhuru wa Korea.
Mwandishi: Najma Said/APE/EAP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman