PARIS:Kansela Schroeder katika ziara ya kuaga
15 Oktoba 2005Matangazo
Ujerumani na Ufaransa katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya utakaofanywa mwisho wa Oktoba nchini Uingereza,zinadhamiria kugombea Ulaya inayoshughulikia jamii.Rais Jacques Chirac wa Ufaransa,wakati wa ziara ya kuaga ya Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani mjini Paris, amesema nchi zote mbili zina mtazamo mmoja kuhusu mustakabali wa Ulaya.Schroeder amesisitiza kuwa Ufaransa na Ujerumani,upande mmoja zinataka kugombea ufanisi wa uchumi na kwa upande mwingine zinataka kuwa na umoja wa kijamii.Kansela Schroeder anaeondoka madarakani amesifu pia uhusiano mzuri uliopo kati ya viongozi hao wawili.