PARIS : Waziri wa Fedha wa Ufaransa ajiuzulu
26 Februari 2005Matangazo
Waziri wa Fedha wa Ufaransa Herve Gaymard amejiuzulu kutokana na kashfa ya nyumba.
Hatua hiyo inakuja kufuatia kubainika kwamba yeye, mke wake na watoto wanane walikuwa wakiishi kwenye nyumba kubwa ya kifahari mjini Paris inayolipiwa na serikali ya Ufaransa kwa gharama za Euro 14,000 kwa mwezi.
Gaymard mshirika wa Rais Jaques Chirac alikuwa ndio kwanza ameshika wadhifa huo hapo mwezi wa Novemba mwaka jana na kashfa hiyo imetokea wakati serikali ikiwa katika mpango wa kubana matumizi.