1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Ripoti ya kifo cha Osama Bin Laden haijathibitishwa

23 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD9e

Gazeti la Kifaransa L´Est Republicain hii leo limeripoti kuwa shirika la upelelezi la Saudi Arabia limepata habari kuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda,Osama Bin Laden,amefariki Pakistan mwezi uliopita,baada ya kuugua homa ya matumbo.Gazeti hilo limesema,ripoti yake imetolewa kuambatana na hati ya siri iliyotoka idara ya upelelezi ya Ufaransa na kuongezea kuwa Rais Jacques Chirac wa Ufaransa amearifiwa juu ya ripoti ya Saudi Arabia.Siku ya Jumamosi,rais Chirac na waziri wake wa ulinzi,Michelle Alliot-Marie walisema,ripoti hiyo haiwezi kuthibitishwa, lakini uchunguzi utafanywa kuhusu ripoti iliyofichuliwa.Afisa wa upelelezi wa Kimarekani ameonya kuwa ripoti hiyo izingatiwe kwa hadhari. Na afisa mmoja katika wizara ya mambo ya ndani nchini Pakistan amesema,serikali ya Islamabad haijapokea habari kutoka serikali yo yote ile ya kigeni kuthibitisha ripoti hiyo.