1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Mkuu wa zamani wa majeshi ya Lebanon kurejea

15 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFWh

.

Mkuu wa zamani wa majeshi ya Lebanon Bwana Michel Aoun anapanga kurejea nchini Lebanon katika muda wa wiki mbili zijazo ili kujitayarisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao mwezi wa May.

Kiongozi huyo mfuasi wa madhehebu ya Kikristo ya Maronite amesema kuwa atakuwa na orodha ya pamoja ya wagombea wa chama chake pamoja na mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Druze, Bwana Walid Jumblatt.

Bwana Aoun aliiongoza serikali ya kijeshi kabla ya kuondolewa madarakani na kwenda kuishi uhamishoni nchini Ufaransa mwaka 1990 kutokana na mashambulizi ya jeshi la Syria na Lebanon.