PARIS: Lebanon kupewa msaada wa Dola bilioni 7.6
26 Januari 2007Matangazo
Jumuiya ya kimataifa imeahidi kuipa Lebanon msaada wa Dola bilioni 7.6 kuijenga upya nchi hiyo.Wajumbe kutoka nchi 40 walitoa ahadi hiyo siku ya Alkhamisi kwenye mkutano wa wafadhila uliofanywa mji mkuu wa Ufaransa,Paris.Saudi Arabia peke yake imearifu kuwa itatoa msaada wa Dola bilioni 1.1.Waziri mkuu wa Lebanon Foaud Siniora pia alihudhuria mkutano huo na aliwaeleza wafadhila mpango wa kutaka kuijenga upya nchi na kufufua uchumi wa nchi hiyo.Siniora anaeungwa mkono na nchi za magharibi amesema,ameridhika na msaada huo wa fedha.