1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Iran inataka kuendelea kurutubisha madini ya uranium.

23 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFUB

Jumuiya ya Ulaya na Iran zimeanza duru nyingine ya mazungumzo ya kinuklia leo, huku Iran ikitishia kujitoa iwapo jumuiya ya Ulaya itaendelea kusisitiza kuwa nchi hiyo iachane na mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium, maada muhimu katika utengenezaji wa bomu la kinuklia.

Ali Agha Mohammadi, msemaji wa baraza la taifa la usalama nchini Iran , amesema kuwa nchi yake inatarajia wapatanishi wa jumuiya ya Ulaya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani watakuwa wanaelewa nia ya Iran ya kurutubisha madini hayo ya uranium.

Nchi hizo tatu za jumuiya ya Ulaya zimeiahidi Iran kufanya nayo biashara, kuipatia teknolojia, na masuala ya usalama, iwapo nchi hiyo itaachana na mpango wake huo wa urutubishaji madini hayo na kuondosha madai ya Marekani kuwa Iran inajaribu kwa siri kuwa na silaha za kinuklia.