PARIS : Chirac ahojiwa katika kashfa ya fedha
20 Julai 2007Matangazo
Hakimu wa Ufaransa amemhoji rais wa zamani wa nchi hiyo Jaques Chirac katika uchunguzi wa kashfa ya fedha katika chama ambayo imeanzia wakati alipokuwa meya wa jiji la Paris.
Kwa zaidi ya masaa manne Chirac alikabiliwa na masuala akiwa kama shahidi na kuna uwezekano kwamba hatimae anaweza kukabiliwa na mashtaka.Uchunguzi huo unaangalia mpango wa ajira wa bandia ambao ulitumiwa kugharimia chama cha kihafidhina cha Chirac RPR wakati akiwa meya kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1995.
Chirac amekanusha kuwa na kosa lolote lile katika kashfa hiyo na hii ni mara ya kwanza kabisa kwamba rais wa zamani wa Ufaransa kuhojiwa katika uchunguzi wa kisheria.