1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Papa Francis kuzuru kisiwa cha Corsica Ufaransa

Saleh Mwanamilongo
24 Novemba 2024

Kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis anatazamiwa kuzuru kisiwa cha Ufaransa cha Corsica mwezi ujao kushiriki katika kongamano la masuala ya kidini Kanda ya Mediterania na kuongoza Misa.

https://p.dw.com/p/4nNHm
Papa Francis kuzuru Ufaransa lakini hatohudhuria ufunguzi wa Notre Dame
Papa Francis kuzuru Ufaransa lakini hatohudhuria ufunguzi wa Notre DamePicha: ANDREAS SOLARO/AFP

Kisiwa hicho hakijawahi kutembelewa na papa. Francis atakutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa ziara yake ya siku moja mnamo Desemba 15. Mkutano huo umepangwa muda mfupi kabla Papa Francis kurejea Roma.

Wiki moja kabla ya ziara ya Papa Francis huko Corsica, Kanisa kuu la Notre-Dame huko Paris litafunguliwa tena kufuatia ukarabati wa muda mrefu baada ya kutetekezwa na moto mwaka 2019.

Hapo awali Macron alitarajia papa kuhudhuria sherehe hiyo kufunguliwa tena wa Kanisa. Lakini mnamo Septemba papa aliweka wazi kwamba hatashiriki.