Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis hii leo anaanza ziara ya siku sita katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Sudan Kusini, ikilenga kuleta ujumbe wa amani kwa mataifa hayo mawili yaliyokumbwa na umaskini, mizozo na kile Francis amekiita mawazo ya kikoloni ambayo bado yanaichukulia Afrika kama bara lililo tayari kunyonywa