SiasaSudan Kusini
Papa Francis kuelekea Sudan Kusini baada ya Congo
3 Februari 2023Matangazo
Baba Mtakatifu Francis ataondoka mjini Kinshasa majira ya mchana baada ya kukamilisha mkutano na maaskofu wa kanisa katoliki nchini Kongo.
Atawasili mjini Juba mnamo saa tisa alasiri ambako amepangiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa kisiasa wa taifa hilo pamoja na kuongoza misa ya kuombea amani.
Akiwa nchini humo, Papa Francis atajiunga na viongozi wa wakuu duniani wa kanisa ya Anglikana na lile la Scotland. Anatarajiwa kutumia ziara hiyo kama ilivyokuwa nchini Congo kuhimiza amani, kusameheana na kukomesha rushwa.
Kiongozi huyo mkuu wa kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis aliwasili katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Jumanne akiwa na ujumbe wa kukomeshwa kwa vita na machafuko.