1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis kuanza ziara nchini Hungary

27 Aprili 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Francis anatarajia kuanza ziara ya siku tatu nchini Hungary, itakayogubikwa na ajenda juu ya vita vya nchini Ukraine, uhamiaji na mizizi ya Ukristu barani Ulaya

https://p.dw.com/p/4Qcsv
Vatikan I Papst Franziskus leitet die Feier der Osternacht
Picha: Gregorio Borgia/AP/picture alliance

Papa Francis atazungumzia masuala hayo atakapohutubia umma na katika mazungumzo yake na waziri mkuu Victor Orban. 

Papa Francis anafanya ziara hii, akitimiza ahadi yake aliyoitoa mwaka 2021, wakati alipokwenda chini humo kwa muda mfupi tu kufunga kongamano la Kanisa mjini Budapest, akiwa njiani kuelekea Slovakia.

Hii ni ziara yake ya kwanza tangu alipolazwa hospitalini kutokana na maambukizi kwenye mapafu mnamo mwezi Machi.

Ingawa lengo lake kuu ni kukutana na Wakatoliki wa Hungary, lakini kiongozi huyo amekiri siku ya Jumapili kwamba lengo hilo litagubikwa na matukio yanayojitokeza sasa.