1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis azuru mtaa wa mabanda, Copacabana

26 Julai 2013

Baba Mtakatifu Francis ambaye yuko ziarani nchini Brazil, amewahutubia vijana wa kikatoliki huku akitoa wito wa kuwepo "mshikamano wa utamaduni" badala ya "uchoyo na ubinafsi" katika jamii ya kisasa

https://p.dw.com/p/19EaR
epa03800925 Pope Francis waves to well-wishers as he arrives at Varginha shanty town in Rio de Janeiro in Brazil, 25 July 2013. Pope Francis is in Brazil for the celebration of the World Youth Day,which runs until 28 July, on his first trip overseas since he was elected. EPA/David Fernandez
Papst Franziskus in Brasilien 25.07Picha: picture-alliance/dpa

Umati mkubwa wa wakatoliki milioni 1.5 ulijitokeza kumsalimia Papa Francis katika ufuo wa Copacabana hapo jana baada ya kiongozi huyo kuzuru mtaa mmoja wa mabanda mjini Rio ili kutuma ujumbe wa kuwatetea watu maskini. Papa huyo anayetokea Ameriak ya Kusini alikabiliwa na picha tofauti za maisha katika mji wa Rio, kutoka upande wa mbele wa ufuoni hadi mitaa ya mabanda katika maeneo ya milima. Papa Francis alirudia tena mada ambayo amekuwa akizungumzia wakati wote wa ziara yake nchini Brazil, ya kuwaomba vijana wa Kikatoliki kuwachana na mitengo ya kupenda vitu vya dunia na kumweka Yesu maishani mwao.

Anasema mali, pesa na mamlaka vinaweza kumfanya mtu kujidanganya kuwa mwenye furaha, lakini huwa vinatutawala na kutufanya tutake kuwa na vingi hata zaidi, bila kuridhika. Maafisa wa kanisa katoliki mjini Vatican hawakuficha ukweli kwamba ziara ya kwanza ya kigeni ya Baba Mtakatifu tangu alipochaguliwa inalenga kuwaongeza nguvu na imani wafuasi wake.

Ziara hiyo inakuja wakati ambapo kumekuwa na mdahalo mkubwa nchini humo ya kuhusiana na maswala ya ufisadi serikalini, ukiuakaji wa sheria vilivyochochea maandamano mitaani.

Waumini wakikatoliki walimkaribisha Papa Francis katika sherehe za Siku ya Vijana Ulimwenguni
Waumini wakikatoliki walimkaribisha Papa Francis katika sherehe za Siku ya Vijana UlimwenguniPicha: AFP/Getty Images

Papa Francis aliwaambia vijana waliokusanyika kuwa wanafahamu vyema kuhusu vitendo vya dhuluma vinavyofanywa nchini mwao, lakini kila mara huwa wanakasirishwa kutokana na ukweli kwamba ufisadi unafanywa na watu wanaoweka mbele matakwa yao tu. Amewataka vijana wakikate tamaa, na wasipungukiwe na imani na kukubali kuzimwa matumaini yao. Mwezi uliopita Brazil ilikumbwa na maandamano makubwa kuwahi kushuhudiwa katika miongo miwili, wakati zaidi ya watu milioni moja walipoingia barabarani kulaani ufisadi, huduma duni za usafiri wa umma na gharama kubwa za kuandaa tamasha la kombe la dunia mwaka ujao 2014. Wakati sherehe za jana za ufuoni, karibu watu 500 walifanya maandamno ya kupinga ufisadi mbele ya jengo la kifahari la gavana wa mji wa Rio.

Mtaa wa Varginha wenye wakaazi 1,000 ni mmoja wa mitaa kadhaa ya mabanda ambayo polisi wameyafurusha magenge ya biashara harau ya dawa za kulevya na kurejesha utulivu kabla ya kombe la dunia hapo mwakani na michezo ya Olimpiki mwaka wa 2016. Chini ya ulinzi mkali, Papa Francis alitembea katika barabara za mtaa huo, huku akisimama ili kuzungumza na wakaazi waliojawa furaha, kuwabusu watoto na kukubali kuvishwa taji la maua shingoni. Alimtembelea mkaazi mmoja nyumbani kwake katika mtaa huo wa mabanda, na kuyabariki madhabahu ya kanisa moja katika eneo hilo. Kisha baadaye Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliwahutubia Wargetina wenzake waliokusanyika kanisani na kuwasilisha ujumbe kuwa wahubiri ni lazima waishi na kufanya kazi yao kama watu wa kawaida.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP

Mhariri: Josephat Charo