1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa arekebisha sheria ya unyanyasaji wa kingono

Angela Mdungu
25 Machi 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis leo amerekebisha sheria ya kanisa ya mwaka 2019 yenye lengo la kuwawajibisha viongozi wa kanisa wanaoficha kesi za unyanyasaji wa kingono.

https://p.dw.com/p/4PF1W
Vatikan Papst Franziskus Rückkehr nach Italien
Picha: Tiziana Fabi/AFP

Papa Francis ameitanua sheria hiyo ili kuwashirikisha pia viongozi walei wa Kikatoliki na kusisitiza kwamba watu wazima pia wanaweza kuwa waathiriwa wa unyanyasaji.

Sheria mpya zinasisitiza kuwa hata watu wazima wanaweza kuwa waathirika wa vitendo vilivyofanywa na makasisi kama vile watawa au wanaseminari ambao wanawategemea maaskofu au wakubwa wao. Awali kanisa liliwazingatia tu watu wazima wenye matatizo ya akili kama wahanga sambamba na watoto.

Sheria mpya zitawachunguza maaskofu wanaotuhumiwa kwa unyanyasaji au kuficha maovu. Aidha, inawapa mamlaka wafanyakazi wote wa kanisa kuripoti kanisani madai ya unyanyasaji ya makasisi, ingawa haiwapi mamlaka ya kuripoti polisi. Pia inawahakikishia ulinzi wanaotoa taarifa za unyanyasaji.

Chanzo: APTN