Papa Francis akamilisha ziara yake nchini Ubelgiji
29 Septemba 2024Matangazo
Misa hiyo imehudhuriwa na waumini wapatao 40,000 kutoka Ubelgiji, Ujerumani, Ufaransa na Uholanzi.
Mchana huu papa anaondoka nchini humo na kurejea Vatikan kufuatia hafla fupi ya maagano kwenye uwanja wa ndege. Mwanzoni mwa misa hiyo, Papa alimtangaza Anne wa Yesu kuwa mtakatifu.
Soma pia:Papa Francis amesema kashfa za unyanyaji watoto kingono ni fedheha kwa kanisa
Mwanamke huyo mwenye asili ya Hispania alikufa huko Brussels mnamo 1621 na alihusika kuanzisha nyumba za watawa katika maeneo kadhaa ikiwemo Antwerp na Tournai.
Mwanamke huyo ambae pia alikuwa mwalimu wa kanisa Katoliki anachukuliwa kuwa moja ya wanawake maarufu katika taasisi hiyo ya kidini ulimwenguni.