1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa akamilisha miaka 5 tangu kuchaguliwa kuliongoza kanisa Katoliki

16 Aprili 2010

Kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani Baba Mtakatifu Benedikti XVI, Jumatatu ijayo tarehe 19 mwezi huu wa Aprili anatimiza miaka mitano tangu ashike wadhifa huo wa kuliongoza kanisa hilo

https://p.dw.com/p/MyVF
Papa Benedict XVIPicha: AP

Baba mtakatifu alizaliwa na kuitwa Josef Ratzinger, mnamo siku ya Jumamosi takatifu ya tarehe 16 mwezi Aprili mwaka 1927 kusini mwa Ujerumani, katika mji mdogo uitwao Marktl Inn unaopatikana kati ya mji wa Munich na mji wa Passau. Babake alikuwa ni afisa wa polisi katika eneo hilo, lakini Josef Ratzinger mwenyewe alikuwa kijana aliyependa mambo ya Mungu na kujiandikisha kwa masomo katika seminari ya Traunstein.

Bila shaka kama kijana alikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kwa kawaida huwakabili vijana, lakini hata hivyo alifanya bidii na kujiendeleza kusomea thioljia katika chuo cha Theolojia cha mjini Munich kusini mwa Ujerumani. Kama binadamu alihuzinishwa na kifo cha babake mnamo mwaka 1959 na pia kifo cha mamake mnamo mwaka 1963, lakini alijipa moyo na kuendelea kufuatilia mambo ya dini.

Mnamo tarehe 28 mwezi Mei mwaka 1977 Josef Ratzinger aliwekwa wakfu kama askofu mkuu wa Munich na Freising. Mnamo Aprili 19 mwaka 2005, alichaguliwa papa kuliongoza kanisa Katoliki na kuchukua jina la papa Benedict wa 16, kumuenzi Mtume Benedict na papa Benedict wa 15, aliyeliongoza kanisa Katoliki wakati wa vita vikuu vya kwanza vya dunia.

Kama kiongozi wa kanisa Katoliki diniani, baba mtakatifu Benedikt wa 16 anatakiwa kuwa mfano hai kwa umoja wa waumini Wakatoliki, lakini pia Wakristo wote duniani.

Je, katika kipindi hiki cha miaka mitano ni mambo gani ambayo kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani ameweza kuyafanikisha katika kipindi hiki cha miaka mitano? Je, ni mchango gani alioutoa katika kuufanya ulimwengu kuwa mahala pazuri zaidi pa kuishi?

Kuyajibu maswali haya pamoja na mengine, tumemualika Askofu Method Kilaini, jimbo la Bukoba nchini Tanzania. Pascal Maziku, Youth Alive Movement, Dar es Salaam, Tanzania.

Na kutoka huko nchini Kenya tunaye bwana Nolasco Kubasu, aliyekuwa zamani mseminari, na ambaye hivi sasa anafanya kazi na idara ya srikali inayohusika na juhudi za kudumisha amani katika mkoa wa bonde la ufa nchini humo.

Na kutoka hapa Ujerumani yuko John Mwakafalili katika mji wa Munich kusini mwa Ujerumani.

Mwenyekiti ni Josephat Charo