Yaliyomo katika Afrika wiki hii ni pamoja na kutangazwa kwa usitishaji vita kwa saa 24 nchini Sudan.Nchini Tanzania sakata linalohusisha tuhuma za serikali kukodisha bandari zake kwa kampuni moja ya Dubai lapamba moto huku bunge likionya vyombo vya habari juu ya kutoa kile ilichokiita habari potofu. Rais Paul Kagame wa Rwanda afanya mabadiliko makubwa katika jeshi. Ungana na Saumu Mwasimba.