1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pande zinazopigana Yemen zabadilishana orodha ya wafungwa

Sekione Kitojo
19 Desemba 2018

Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu limesema pande zinazopigana Yemen zimebadilishana orodha ya majina ya watu karibu 16,000 waliokamatwa kama sehemu ya kubadilishana wafungwa makubaliano yaliyofikiwa wiki iliyopita

https://p.dw.com/p/3AONf
Schweden Friedensgespräche für Jemen starten vor Drohkulisse
Picha: Reuters/TT News Agency/S. Stjernkvist

Wakati  huo  huo muungano wa  kijeshi  unaoongozwa  na  Saudi Arabia  ulishambulia  kituo cha jeshi la  anga  katika  mji  mkuu  unaoshikiliwa  na  waasi  leo  wakati usitishaji  mapigano  ukiendelea  katika  mji  wa  bandari  wa Hodeida. Sekione Kitojo  na  taarifa  zaidi.

Schweden UN Jemengespräche in Stockholm l Abreise von Rebellenmitgliedern in Sanaa
Ujumbe wa Wahouthi katika mkutano wa Sweden ukiwasili Picha: Reuters/M. Al-Sayaghi

Kundi  la  Wahouthi wenye  mafungamano  na  Iran  na  serikali  ya Yemen  inayoungwa  mkono  na  Saudi  Arabia  wanatarajiwa kuwaachia  huru  wafungwa  kwa  wakati  mmoja  mwezi  ujao kama sehemu  ya  kujenga  hali  ya  kuaminiana  iliyofikiwa  katika makubaliano  katika  mazungumzo  ya  amani  yaliyosimamiwa  na Umoja  wa  Mataifa  nchini  Sweden. 

Mkurugenzi  wa  kanda  wa shirika  la  msalaba  mwekundu, Fabrizio carboni, kwamba pande zinazohusika zimebadilishana  orodha  ya wafungwa.

Jemen | Huthi Rebellen
Wapiganaji wa Kihouthi nchini YemenPicha: picture alliance/dpa/Y. Arahab

"Wana wiki sita kuanzia sasa  kuhakikisha  kwamba  orodha  hizo  ni sahihi na  watu  hao  wanashikiliwa. Kwa hiyo itatuchukua  hadi katika  wiki  ya  kwanza  ya  januari  ambako  watakuwa  na  siku kumi  kuwaachia  wafungwa  na  kuwapeleka  katika  maeneo  yao ya  asili."

Muungano wa  kijeshi

Operesheni  hiyo inaulazimu  muungano  wa  kijeshi  unaoongozwa na  Saudi  Arabia  kuhakikisha  kwamba  anga  ni  salama kwa  safari za  ndege, amesema  Carboni.

Fabrizio Carboni Rotes Kreuz Libanon
Mkurugenzi wa kanda wa shirika la msalaba mwekundu Fabrizio CarboniPicha: ICRC

Wakati  huo  huo  pande  hizo  zinazopigana  zimelaumiana  kwa kukiuka  makubaliano  ya  kusitisha  mapigano  mjini  Hodeida yaliyofikiwa  kwa  upatanishi  wa  Umoja  wa  Mataifa yenye  lengo la  kuepuka  vita  kamili  kuwania  udhibiti  wa  bandari  hiyo inayotumika  kwa  kuingiza  misaada  muhimu  na  kusafisha  njia kwa  ajili  ya  majadiliano  zaidi  ya  amani.

Wakaazi  wameripoti  kuhusu  mashambulio  ya  anga jana Jumanne, lakini  duru  katika  muungano  unaoongozwa  na  Saudi Arabia  zimeliambia  shirika  la  habari  la  Reuters  kwamba  iwapo waangalizi  wa  kimataifa  hawatawekwa  mjini Hodeida  hivi karibuni, makubaliano  hayo  ya  kujenga  kuaminiana  huenda yakashindwa.

Martin Griffiths UN Sonderbeauftragter Jemen
Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa nchini Yemen Martin Griffith akiwasili katika uwanja wa ndege wa Sanaa nchini YemenPicha: Reuters/M. Al-Sayaghi

Hodeida, bandari  kuu inayotumika  kuwalisha  watu  milioni 30 wa Yemen, imekuwa  lengo  la  mapigano  mwaka  huu, na  kuzusha hofu  nje ya  nchi  hiyo kwamba  iwapo  vita  kamili  vikitokea inaweza  kuzuwia  watu  milioni  15.9 kupata  mahitaji  yao  na kusababisha  matatizo  makubwa  na  njaa.

Mwandishi: Sekione  Kitojo/rtre/afpe

Mhariri: Mohamed Khelef