Pande hasimu Sudan zilikutana kwa siri mara tatu Bahrain
1 Februari 2024Matangazo
Haya yamesemwa na vyanzo vinavyofahamu mazungumzo hayo. Kulingana na vyanzo hivyo vinne, ambapo viwili vilikuwa kwenye mazungumzo hayo, mikutano hiyo ya Manama ilihudhuriwa manaibu wakuu wenye ushawishi kutoka pande zote mbili na maafisa kutoka Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Mazungumzo hayo ambayo hayakutangazwa, yalihudhuriwa pia na maafisa wa Marekani na Saudi Arabia.
Soma pia:Pande zinazozozana za Sudan zinafanya uhalifu Darfur-ICC
Haya yanafanyika wakati ambapo kumekuwa na majaribio ya mara kadhaa ya nchi hizo na hata mataifa ya Afrika Mashariki kujaribu kutafuta suluhu la mzozo huona kusitishwa kwa mapigano.