1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PALERMO: Wakimbizi wamezama karibu ya Sicily

12 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEcB

Watu 11 waliotaka kukimbilia Ulaya,wamezama walipokuwa wakiogelea kuelekea kisiwa cha Sicily nchini Italia.Walinzi wa pwani wa Kitaliana walikuta maiti baada ya kuiokoa mashua ya uvuvi iliyokuwa ikizama ikiwa na zaidi ya watu 70.Kuna khofu kuwa wengine 50 wanakosekana.Idadi fulani ya watu miongoni mwa wale walionusurika wamekamatwa,wakishukiwa kuhusika na kazi ya kusafirisha binadamu kwa magendo.Wale waliopona wamewaambia maafisa wa Kitaliana kwamba walikuwa njiani muda wa siku tatu baada ya kuondoka kaskazini mwa Libya.Katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo ya mwaka huu,zaidi ya wakimbizi 7,500 wamekamatwa kwa sababu ya kuwasili katika pwani za Italia,kinyume na sheria.