PALE : Vikosi vya NATO vyavamia nyumba za watoto wa Karadzic
20 Februari 2007Matangazo
Vikosi vya Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO wamezivamia nyumba za mtoto wa kiume na binti wa mtuhumiwa wa uhalifu wa vita wa Serbia ya Bosnia Radovan Karadzic.
Msemaji wa NATO amesema Sonja na Sasa Karadzic wamehojiwa juu ya mahala alipo baba yao.Msako huo kwenye mji wa Bosnia wa Pale ambao uko kama kilomita 15 mashariki ya Sarajevo unafuatia repoti za ujasusi kwamba watoto hao wawili wanahusika na mtandao wa kumsaidia baba yao.
Hii sio mara ya kwanza kwa watoto hao kuhojiwa kuhusiana na msako wa baba yao ambaye mahkama ya uhalifu wa vita ya Umoja wa Mataifa inamshtaki kwa mauaji ya kimbari wakati wa vita vya Bosnia kuanzia mwaka 1992 hadi mwaka 1995.