1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ozil ajiunga Real Madrid, Anelka afungiwa mechi 18

Aboubakary Jumaa Liongo17 Agosti 2010

Real Madrid imetangaza kumsajili kiungo wa kimataifa Ujerumani Mesut Ozil kutoka klabu ya Werder Bremen.

https://p.dw.com/p/OpeP
Mesut Oezil wa Werder BremenPicha: AP

Mtandao wa klabu hiyo umesema kuwa Ozil aliyetamba katika fainali za kombe la dunia huko Afrika Kusini, ameingia mkataba na timu hiyo wenye thamani ya Euro millioni 15.

Anaungana na kiuongo mwengine wa Ujerumani Sami Khedira, katika kikosi hicho kinachosukwa na Jose Morinho.Khedira alikuwa akichezea VfB Stuttgart.

Ozil ambaye ni mjerumani mwenye asili ya kituruki alijiunga na Werder Bremen mwaka 2008 akitokea Schalker 04 na amefunga mabao 12 katika mechi 71 za Bundesliga alizocheza.

Nchini Ufaransa, Shirikisho la soka la nchi hiyo FFF limetangaza kumfungia mshambuliaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo na klabu ya Chelsea Nicolas Anelka mechi 18 kuichezea timu ya taifa, kwa kosa la kumtusi kocha wa timu ya Ufaransa Raymond Domenech wakati wa fainali za dunia huko Afrika Kusini.

Pia nahodha wa timu hiyo ya Ufaransa Patrice Evra amefungiwa mechi tano kwa kosa la kuongoza wachezaji kugomea mazoezi wakati wa fainali hizo.

Shirikisho hilo la Soka la Ufaransa apia limemfungia mechi tatu kiungo wa nchi hiyo anayechezea Bayern Munich Frank Ribbery.Katika fainali hizo za dunia huko Afrika Kusini, Ufaransa iliondoshwa katika hatua ya awali

Mwandishi:Aboubakary Liongo