1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Oxfam: Matajiri duniani waongeza utajiri wao

25 Julai 2024

Shirika la misaada la Oxfam limesema Alhamis kuwa asilimia moja ya watu matajiri duniani wameongeza utajiri wao kwa jumla ya dola trilioni 42.

https://p.dw.com/p/4iiJK
Elon Musk in Bali
Picha: Sonny Tumbelaka/AFP

Hili limefanyika katika muda wa muongo mmoja uliopita.

Takwimu hizo zimetolewa kuelekea mkutano wa kilele wa mataifa yaliyoendelea kiviwanda G20, nchini Brazil ambapo utozaji ushuru kwa matajiri wakubwa duniani ni moja ya ajenda kuu ya mkutano huo.

Oxfam imetahadharisha kuwa pengo kati ya matajiri na maskini huenda likawa kubwa zaidi.

Brazil ambayo ilichukua urais wa kupokezana wa G20 mnamo Disemba mwaka jana, iliweka moja kati ya vipaumbele vyake kuwa ni kuwatoza ushuru matajiri wa kupindukia.

Katika mkutano wa kilele wiki hii mjini Rio de Janeiro, mawaziri wa fedha wa G20 wanatarajiwa kujadili juu ya njia za kuongeza ushuru kwa matajiri wakubwa duniani na kuziba mianya ya watu kukwepa mifumo ya kodi.