OTTA / NIGERIA: Rais Rbert Mugabe hataalikwa katika mkutano wa Commonwealth-
25 Novemba 2003Matangazo
Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria, amesema Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe hatahudhuria mkutano ujao, wa jumuia ya madola "Commonwealth", ya Uingereza na koloni zake za zamani- Rais Obasanjo, amesema Rais Robert Mugabe hakualikwa katika mkutano huo, unaotazamiwa kufanyika nchini Nigeria, mwezi ujao wa December. Swali kuhusu ikiwa Rais Robert Mugabe angehudhuria mkutano huo wa Jumuia ya "Commonwealth", limezusha mgawanyiko mkubwa miongoni mwa nchi wanachama, kutokana na uhusiano mbaya uliyopo baina ya serikali ya Rais Robert Mugabe na Uingereza. Nchi hio, pamoja na Australia, zinashutumu Rais Robert Mugabe kuendesha utawala wa mabavu na kunyanyasa wapinzani. Chanzo cha uhusiano huo uliozorota, ni mradi wa serikali ya Zimbabwe, uliopokonya wakulima wa kizungu wa nchi hio, mashamba ya kulima, na kuyagawa kwa raia weusi.