OSLO:Shirika la nishati ya Atomiki IAEA na mkurugenzi mkuu wake washinda tunzo ya Nobel 2005
7 Oktoba 2005Matangazo
Kamati ya tunzo ya amani ya Nobeli mjini Oslo imetangaza hivi punde kwamba Shirika la kimataifa la nguvu za atomiki na mkurugenzi wake mkuu Mohammad El Baradei ndiyo washindi wa tunzo hiyo ya amani 2005.
Taarifa ya kamati hiyo imesema Shirika hilo na Bw El Baradei wametunzwa tunzo hilo kutokana na juhudi zao za kuzuwia nishati ya kinuklia kutumiwa kwa makusudio ya kijeshi na kuhakikisha kwamba nishati ya kinuklea inayotumiwa kwa madhumuni ya amani, inakua ni katika hali ya usalama kwa kiasi kinachowezekana.