OSLO:Shirika la Atomiki IAEA na mkurugenzi mkuu wake ndio washinda tunzo ya amani ya Nobel
7 Oktoba 2005Matangazo
Shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya Atomiki na mkurugenzi mkuu wake Mohammad El Baradei ndio washindi wa ya tunzo ya amani ya Nobeli ya mwaka 2005.
Ushindi huo umetangazwa hii leo mjini Oslo na kamati ya tunzo hiyo.
Taarifa ya kamati hiyo imesema Shirika hilo na Bw El Baradei wametunzwa tunzo hilo kutokana na juhudi zao za kuzuwia nishati ya kinuklia kutumiwa kwa makusudio ya kijeshi na kuhakikisha kwamba nishati ya kinuklea inayotumiwa kwa madhumuni ya amani, inakua ni katika hali ya usalama kwa kiasi kinachowezekana.