OSLO:Hisia mbali mbali juu ya Ushindi wa IAEA na mkurugenzi wake mkuu wa tunzo ya amani ya Nobel
7 Oktoba 2005Viongozi mbali mbali wameeleza hisia zao kufuatia ushindi wa tunzo ya Nobel wa shirika la IAEA Na mkurugenzi wake Mohammad El Mutasa.
Akizungumzia juu ya ushindi huo naibu waziri mkuu wa Israel Shimon Peres amesema hii ni ishara inayotoa onyo kwa Iran juu ya mpango wake wa Nuklia.
Kansela Gerhard Schröder amesema tunzo ya Nobel kwa Elbaradei na shirika la kudhibiti nishati ya Atomiki ni uamuzi wa makini.
Ameongeza kusema kwamba ushindi huo umetokana na kazi iliyokuwa ikifanywa na Elbaradei na shirika hilo wakati wa vita vya Iraq pamoja na jitihada zake za kutatua mzozo wa Iran kwa njia za kidiplomasia.
Wakosoaji wa ushindi huo wa tunzo ya Nobel kama vile kikundi cha Ufaransa kinachojishughulisha na harakati za kuachana na matumizi ya Nuklia wanasema shirika la IAEA pamoja na mkurugenzi wake mkuu Mohammed El Baradei wameshindwa kuzuia kusambaa kwa silaha za Nuklia.