OSLO: Tuzo ya Amani ya Nobel kwa IAEA na El Baradei
8 Oktoba 2005Matangazo
Tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2005 imetolewa kwa Shirika la Nishati ya Kunuklia la Umoja wa Mataifa-IAEA na Mkurugenzi wake mkuu Mohamed ElBaradei alie mzaliwa wa Misri.Halmashauri ya Nobel imenukuu mchango wa Shirika hilo la Umoja wa Mataifa kusaidia kupunguza utapakaji wa silaha za kinuklia na kuhakikisha matumizi ya usalama ya nishati ya kinuklia.Mjini Vienna kwenye mkutano pamoja na waandishi wa habari,ElBaradei alisema ,Tuzo ya Amani ya Nobel inaimarisha azma yake.