1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

OSLO: Japan yaahidi msaada wa dola milioni 100 kwa Sudan.

11 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFOI

Wizara ya mambo ya nje ya Japan imesema kuwa serikali ya japan itaipa msaada wa dola milioni 100 Sudan.

Ahadi hiyo imetolewa na seriakli ya Japan katika mkutano wa kimataifa unaoendelea huko Norway wenye azma ya kukusanya dola bilioni 2.6 za kuisaidia Sudan katika mpango wake wa amani uliotiwa saini mapema mwaka huu na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 21 kati ya kaskazini na kusini mwa Sudan.

Serikali ya washington imeongeza uzito wake katika mkutano huu kwa kumtuma muwakilishi wake huko Oslo huku baadhi ya mataifa fadhili yakionya kuwa misaada haitatolewa ikiwa serikali ya Khartoum haitakomesha ghasia za Darfur, ambako maelfu ya watu wamepoteza maisha na wengine zaidi ya milioni mbili wamelazimika kuyahama makaazi yao kufuatia mashambulizi ya wanajeshi wa Janjaweed ambao inadaiwa wanaungwa mkono na serikali ya Khartoum.