1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Oscar Pistorius aachiwa kwa dhamana

Abdu Said Mtullya22 Februari 2013

Mwanamichezo maarufu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius anayekabiliwa na mashtaka ya kuua kwa kudhamiria ameachiwa kwa dhamana na mahakama mjini Pretoria

https://p.dw.com/p/17kJ9
Olympic athlete Oscar Pistorius stands inside the court as a police officer looks on during his bail hearing at the magistrate court in Pretoria, South Africa, Wednesday, Feb. 20, 2013. A South African judge says defense lawyers will need to offer "exceptional" reasons to convince him to grant bail for Oscar Pistorius, when a hearing resumes Wednesday. (AP Photo/Themba Hadebe)
Pistorius vor GerichtPicha: picture alliance / AP Photo

Mahakama ya mjini Pretoria inayosikiliza mashtaka yanayomkabili mwanamichezo maarufu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius imeyakubali maombi ya mwanamichezo huyo ya kuachiwa kwa dhamana.

Kwa mujibu wa taarifa mwanamichezo huyo alionekana akiyatikisa mabega yake wakati hakimu alipoanza kusoma maombi yake ya kuachiwa kwa dhamana. Hapo awali Jaji huyo Desmond Nair alimwuuliza Pistorius "jee upo sawa"?

Hakimu huyo aliyasoma maelezo ya kina kirefu ya Pistorius juu ya matukio yaliyotukia katika usiku ambapo mpenzi wake Reeva Steenkamp aliuawa nyumbani kwa Pistorius. Mwanamichezo huyo alifikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kuua kwa kudhamiria.

Mwendesha mashataka Mkuu Gerie Nel alipinga Pistorius kuachiwa kwa dhamana kwa sababu ameeleza kuwa mtuhumiwa anazo fedha na uwezo wa kukimbia nchi. Mwendesha mashtaka huyo ameeleza kuwa japo Pistorius hajasema kuwa anakusudia kukimbia nchini,lakini anatambua kwamba upo wa uwezekano wa kuhukumiwa kifungo.Waendesha mashtaka wanasema Pistorius anayo hatia ya kuua kwa kudhamiria. Na ikiwa atapatikana na hatia hiyo anawezza kupewa hukumu ya kifungo cha maisha jela.

Hata hivyo mwanamichezo huyo ameyakana mashataka ya kuua kwa kudhamiria.Amesema kuwa alimuua mpenzi wake Steenkamp kwa kumpiga risasi bafuni kwa makosa akifikiri alikuwa mwivi alieingia ndani ya nyumba.

Jamaa za Oscar Pistorius wakishangilia uamuzi wa mahakama
Jamaa za Oscar Pistorius wakishangilia uamuzi wa mahakamaPicha: Reuters

Muda mfupi kabla ya uamuzi wa kupewa dhamana kuanza kusikilizwa wakili wa Pistorius alikiri kwamba mteja wake anaweza kuhukumiwa kifungo jela. Lakini wakili huyo ameyakana mashtaka ya kuua kwa kudhamiria yanayomkabili mteja wake.Amekiri kwamba anaweza kukabiliwa na mashtaka ya uahalifu wenye uzito wa chini. Wakili huyo amesema pana uwezekano kwa Pistorius kuhukumiwa kwa kosa la kuua ,lakini siyo kwa kudhamiria.

Wakati huo huo wanasheria wamesema kuwa waendesha mashtaka wameshindwa kutoa hoja zenye nguvu ili kuweza kumweka Pistorius ndani kwa muda wote mpaka wakati wa kutolewa hukumu.

Chini ya sheria za Afrika ya Kusini mtu yeyote aneua bila ya kuwapo tishio lolote anaweza kukabiliwa na mashtaka ya kuuua bila ya kudhamiria.Pistorius ambae wakati wote ameonekana kuwa mtu mwenye masikitiko makubwa kizimbani amekonda na ameanza kutokwa mvi na mara kwa mara anatoa machozi.

Mahakama imeamua kumwachia mwanamichezo huyo maarufu kwa dhamana ya dola 113,000na atafikishwa tena mahakamani tarehe nne mwezi wa juni.

Mwandishi: Mtullya Abdu.Afpe rtre

Mhariri:Josephat Charo