Osama Bin Laden atoa vitisho kuhusu hali ya palestina
21 Machi 2008DOHA
Kituo cha televieheni cha Kiarabu Al Jazeera kimetangaza ukanda wa sauti ya kiongozi wa kundi la mtandao wa kigaidi wa Alqaeda Osama Bin Laden.Katika uknda huo Osama Bin Ladena amezungumzia suala la Palestina akisema hali katika eneo hilo haiwezi kutatuliwa kwa mashauriano bali inawezekana tu kwa mtutu wa bunduki na mkono wa chuma. Ametoa mwito kwa waislamu kuwaunga mkono wanamgambo nchini Iraqna vile vile Palestina.Aidha amewashutumu viongozi wa nchi za kiarabau kwa kuunga mkono mashambulio ya waisraeli dhidi ya eneo la Ukanda wa Gaza linalodhibitiwa na chama cha Hamas. Jumatano tovuti moja ilipeperusha ukanda mwingine wa sauti ya Osama Bin Laden akitishia kuuadhibu Umoja wa Ulaya kwa kuchapisha picha za katuni zinazomkejeli mtume Mohammed.Marekani ilithibitisha kwamba sauti hiyo inawezekana kuwa ni ya Osama Bin Laden na kwamba yuko hai.