OSAKA: Defar wa Ethiopia ashinda medali ya dhahabu
1 Septemba 2007Matangazo
Mshika rekodi ya dunia,Meseret Defar wa Ethiopia amejinyakulia medali ya dhahabu katika mbio za wanawake za mita 5,000 mjini Osaka,kwenye Mashindano ya Riadha Ulimwenguni.Mkenya Vivian Cheruiyot,ameshika nafasi ya pili na mwananchi mwenzake,Priscah Jepleting Cherono ametokea wa tatu katika mbio hizo za mita 5,000.