1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Orbán kufanya uhamiaji kuwa lengo la urais wa Hungary kwa EU

23 Juni 2024

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán ameviambia vyombo vya habari vya Ujerumani kuwa suala la uhamiaji anataka kulipa umumihu mkubwa katika ngwe ijayo ya kushika kiti cha uras wa Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4hOnp
Waziri Mkuu wa Hungary Orban, Budapest
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban akitoa hotuba yake Hungary, mjini Budapest, Hungary, Aprili.25, 2024Picha: SZILARD KOSZTICSAK/EPA

Katika taarifa iliyochapishwa leo hii, anakarabisha mawazo ya Kansela Olaf Scholz, ambae yupo katika tafakari ya wazo la kufanikisha taratibu za kutoa hifadhi kwa mataifa ya nje ya Umoja wa Ulaya.

Itakumbukwa katikati ya Juni, Mahakama ya Ulaya ya Haki (ECJ) iliamuru Hungarykulipa faini ya dola milioni 216 na milioni 1 zaidi kwa siku kwa kutotekeleza uamuzi wa ulitolewa awali wa kubadilisha sera yake ya uombaji hifadhi. Urais wa Umoja wa Ulaya unafanyika kwa mzunguko wa miezi sita na Hungary kuchukua jukumu kutoka kwa Ubelgiji Julai Mosi.