JangaUlaya
Ujerumani yasitisha zoezi la kuwaokoa mabaharia waliopotea
25 Oktoba 2023Matangazo
Meli hiyo ilizama baada ya kugongana na meli nyingine pia jana Jumanne kusini magharibi mwa visiwa vya Helgoland.
Mtu mmoja alithibitishwa kufariki kwenye mkasa huo na wawili waliokolewa.
Kulingana na chama cha waokoaji cha Ujerumani (DGzRS), operesheni ya kuwatafuta mabaharia hao ilisimamishwa usiku na haitaendelea leo.
Soma pia:Kadhaa hawajulikani walipo baada ya ajali ya meli Ujerumani
Meli iliyozama iliyosajiliwa Uingereza ilikuwa imebeba vyuma kutoka Bremen Ujerumani kupeleka Immingham Uingereza, na pia ilikuwa na mafuta, meta za ujazo 1, 300. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.