1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Operesheni dhidi ya magaidi wa al-Qaeda Irak

3 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1aS

BAGHDAD:

Waziri Mkuu Nouri al-Maliki wa Irak ametangaza operesheni kuu dhidi ya magaidi kaskazini mwa nchi.Ametangaza hatua hiyo kufuatia umwagaji mkubwa wa damu uliotokea sokoni siku ya Ijumaa katika mji mkuu Baghdad.Watu 99 waliuawa katika miripuko hiiyo miwili ya bomu.Waziri Mkuu al-Maliki alipouzuru mji wa Mosul kaskazini mwa Baghdad alisema,wakati umewadia kuchukua hatua hiyo muhimu dhidi ya magaidi wa al-Qaeda.