Ongezeko la bei na uviko ndio sababu za umasikini Asia
24 Agosti 2023Matangazo
Kwenye ripoti yake iliyoachapishwa Alhamis, Benki ya Maendeleo ya Asia imesema ingawa Asia na Pasifiki zinajikwamua kurejea katika hali ya kawaida baada ya janga la UVIKO-19, lakini kupanda kwa gharama za maisha kunadidimiza juhudi za kukabiliana na umasikini.
Mchumi mkuu wa benki hiyo ya ADB Albert Park amesema benki hiyo inakadiria watu milioni 155.2 miongoni mwa idadi jumla ya watu kwenye ukanda huo waliishi katika hali hiyo na huenda watu milioni 67.8 wasingeathirika kama majanga hayo yasingalitokea.
Benki hiyo yenye makao yake Manila, inauainisha umasikini wa kupindukia kuwa ni wa chini ya dola 2.15 kwa siku kulingana na mfumuko wa bei uliorekebishwa wa mwaka 2017.