Olaf Scholz ateuliwa kuwa waziri mpya wa kazi.
21 Novemba 2007Matangazo
Berlin. Rais wa Ujerumani Horst Köhler amemteua rasmi Olaf Scholz, katibu mkuu wa zamani wa chama cha Social Democrats, kuwa waziri mpya wa kazi. Mbunge huyo , ambaye hana uzoefu wa uongozi wa serikali, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Franz Muentefering ambaye alijiuzulu kutoka serikali Novemba 13 ili kupata muda zaidi wa kumhudumia mkewe ambaye ni mgonjwa. Muentefering pia alijiuzulu kuwa makamu kansela wa baraza la mawaziri la Angela Merkel. Wadhifa huo umekwenda kwa waziri wa mambo ya kigeni Frank-Walter Steinmeier.