Matangazo
Mwito huo umetolewa wakati Kanisa Katoliki nchini Kenya likiwa limetangaza litawaleta pamoja Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta katika mazungumzo yatakayolenga kumaliza mzozo wa kisiasa ulioko nchini humo. Hata hivyo, hisia za kwamba taasisi za kitaifa zinakosa kuwa na uhuru wa kutekeleza shughuli zake ni jambo ambalo linatatiza juhudi hizi, hata kuibua mgawanyiko baina ya viongozi wa makanisa na wananchi kwa ujumla. Kwa mengi zaidi msikilize mwandishi wetu kutoka Nakuru Wakio Mbogho.