1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama atoa msimamo wa Marekani kuhusu mgogoro wa mashariki ya kati

20 Mei 2011

Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza Katika hotuba yake kuwa kuna umuhimu wa kuusema ukweli na kwamba Palestina na Israel hazina budi kuwa majirani kwa kuizingatia mipaka iliyowekwa mwaka 1967.

https://p.dw.com/p/11KFw
Rais Barack Obama, akitoa hotuba kuhusu mashariki ya katiPicha: AP

Wachambuzi wanasema hotuba hiyo itakuwa imshangaza sana kiongozi huyo wa Israel, na kwamba ni ishara mbaya katika ziara yake hiyo ya siku sita nchini Marekani ambayo inaanza leo kwa kutarajiwa kuwa na mkutano katika Ikulu ya Marekani.

Obama amevurugikiwa kutokana na Netanyahu kukwamisha mazungumzo ya amani, ambayo yalisimama muda mfupi baada ya kuanzishwa Septembaer 2010 kuhusu suala linaloendelea la Israel kuendelea na ujenzi wa makaazi ya Wayahudi katika maeneo ya Wapalastina.

Katika hotuba yake hiyo, Obama alielezea kwa ufafanuzi sera ya Marekani kwa nchi za Mashariki ya Kati kufuatia vuguvugu katika maeneo hayo, lakini alijikita zaidi katika mgogoro wa Israel na Palestina na kutoa wito wa mpango huo wa amani kufanikishwa kwa kuzingatia mipaka iliyokuwepo kabla ya vita vya siku sita vya mwaka 1967.

Mwandishi Itamar Eichner amesema Netanyahu hakutarajia kama Rais Obama angaliweza kutoa hotuba ya uhakika na masharti kwa wakati huu.

Benjamin Netanyahu Wikileaks veröffentlicht Dokumente US Außenpolitik
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: AP

Katika kauli yake, Netanyahu anasema kwamba Marekani iliihakikishia Isreale mwaka 2004 wakati wa utawala wa rais George Bush kwamba "ukweli mpya uliopo sasa" hauwezi kuirejesha mamlaka hiyo katika mipaka ya 1967.

Katika maandiko yake mwandishi Eichner anasema hii ni mara ya kwanza kwa Waziri Mkuu wa Israel kumkemea rais wa Marekani.

Kwa upande wa chama cha Republican nchini Marekani, mshindani mkubwa katika kinyang'anyiro cha urais wa nchi hiyo mwaka 2012, gavana wa zamani wa mkoa wa Massachusetts, Mitt Romney, amemtuhumu Barack Obama kwa kuisaliti Israel, mshirika madhubuti wa nchi hiyo, katika jitihada zake za muda mrefu na mfupi katika kufikia amani ya mashariki ya kati.

Gavana huyo wa zamani amesema " Rais Obama amewatupa Wa-Israeli nje ya Basi", ameidharu Israel pamoja na jitihada zake katika kufanikisha amani.

Gavana hiyo wa zamani pia ameongeza kwamba Obama amevunja kanuni ya mwanzo kabisa ya Marekani ya sera zake za mambo ya nje ambayo inasimamia kuwalinda marafiki zake.

Waziri Mkuu wa Israel anatarajiwa kukutana na Kundi lenye kutoa ushawishi kwa niaba ya Waisrael nchini Marekani, AIPAC, na baadae kulihutubia bunge la pamoja, Congress, ambalo linadhibitiwa na Chama cha Republican, na ambalo limemlaumu Obama kuhusu muelekeo wake katika uhusiano na Israel

Mwandishi Sudi Mnette// AFP

Mhariri: Miraji Othman