1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

090911 USA Obama Arbeit

9 Septemba 2011

Tatizo kubwa linalomkabili rais wa Marekani Barack Hussein Obama ni ukosefu mkubwa wa nafasi za ajira. Obama anataka kuanzisha juhudi za ujenzi wa nafasi mpya za ajira.

https://p.dw.com/p/12Vyd
Rais Barack Obama wa Marekani ambaye alitoa hotuba muhimu jana kuhusu ajira.Picha: AP

Tatizo kubwa linalomkabili rais wa Marekani Barack Hussein Obama ni ukosefu mkubwa wa nafasi za ajira. Kwa kuwa watu wachache wameajiriwa , kwa hiyo watu wachache wanalipa kodi, nguvu kazi chache inatumika, na inakuwa vigumu kuchukua hatua za kufufua uchumi , na ukweli ni kwamba watu wengi wamefutwa kazi. Obama anataka kuuvunja mzunguko huu kwa kuanzisha juhudi za ujenzi wa nafasi za kazi, kama alivyosema katika hotuba yake jana Alhamis. Pamoja na hayo lakini anahitaji kuungwa mkono na chama cha upinzani cha Republican, na hapa ndipo kwenye tatizo lake kubwa la pili.

Kuna zaidi ya asilimia 9 ya watu wasiokuwa na kazi, uchumi unaoyumba yumba, umaarufu unaoporomoka, hayo yote hayakustahili kuwapo wakati rais Obama alipohutubia baraza la Congress jana. Lakini Obama alionekana kuwa ana nia ya kuendelea kupambana , na amewashangaza wasikilizaji wake. Hususan kutokana na jina alilozipa harakati zake hizo , hatua za kupata ajira, ambapo zina thamani ya dola karibu bilioni 450, ilikuwa kwa kweli ni kubwa kuliko ilivyotarajiwa.

Kwa msisitizo mkubwa , rais wa Marekani amewataka wabunge wa upinzani kutoka chama cha Republican kuunga mkono mpango wake huo wa maendeleo.

"Pamoja na tofauti zetu tulizokuwa nazo hapo zamani, mbali ya tofauti zetu za mawazo tutakazokuwa nazo hapo baadaye. Mpango huu ndio mpango sahihi kwa hivi sasa. Mnapaswa kuuidhinisha. Na nitapeleka ujumbe huu katika kila eneo la nchi hii".

Mnapaswa kuupitisha , mara tano Obama alirudia maneno haya katika hotuba yake akitoa wito kwa wabunge wa chama cha Republican. Kiini cha mpango wake , kama ilivyotarajiwa ni kupunguza kodi kwa wafanyakazi na makampuni, ili kuvutia uwekezaji katika ujenzi wa miundo mbinu na kuongeza kodi kwa matajiri. Na kisha, ambapo kwa Obama hili lilikuwa muhimu, mpango huo hautakuwa chanzo cha kuliingiza taifa hilo katika madeni zaidi.

Hatua za kujenga nafasi za ajira, hazitaongeza nakisi, zitalipa.

Kwa hiyo kutakuwa na kile kinachoitwa kamati maalum, ambayo itaanza kazi kwa mara ya kwanza , ili kutafuta fedha kwa ajili ya wafanyakazi. Baraza la Congress lilikuwa na mvutano wiki chache zilizopita kati ya wabunge wa chama cha Democratic na Republican kuhusiana na kuweka mpaka wa kiwango cha serikali kuweza kukopa, katika hatua za kubana matumizi. Mpango huu wa kubana matumizi rais Obama anataka upanuliwe zaidi , ili kuweza kugharamia mpango wake wa kutengeneza nafasi za ajira.

Katika hilo rais Obama anataka kutoa pendekezo la uwezekano wa kubana matumizi. Na ametoa tahadhari kwa wanachama wa chama chake , kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo ni muhimu kwa chama cha Democratic. Kwa hiyo ni lazima kwa mfano kufanyiwa mabadiliko bima ya afya kwa wazee.

Wabunge wa chama cha Republican hata hivyo kabla ya hotuba hiyo ya Obama wameamua kuwa hawatakubaliana naye kabisa. Hii ni baada ya hotuba za spika wa mabaraza yote ya Congress hali ambayo si ya kawaida. Hata hivyo hali ni wazi kwamba iwapo kutakuwa na hatua ya kupandisha kodi, chama cha Republican hakitakubaliana na hilo. Kwa kiasi fulani sehemu ya mpango huo una nafasi ya kukubalika, lakini ni pale tu Warepublican watakapounga mkono.

US Senat Obama
Kikao cha baraza la Congress nchini Marekani. Wajumbe wakimsikiliza rais Obama .Picha: picture-alliance/dpa

"Swali ni kwamba, katika hali inayoendelea ya mzozo wa kitaifa, tunaweza kuacha malumbano ya kisiasa na kufanya kitu kusaidia ujenzi wa uchumi".

Rais Obama ameonya moja kwa moja kwa kila mbunge wa chama cha Republican, kama alivyosema, kwa kuwa kuna mawazo tofauti, nyie mtawaamulia wapiga kura kile kilicho sahihi na kile ambacho si sahihi.

Mwandishi : Büllmann, Rolf / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Josephat Charo