1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama asema makubaliano yamefikiwa

Aboubakary Jumaa Liongo1 Agosti 2011

Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza kuwa wabunge wamekubaliana juu ya mpango wa kuongeza uwezo wa nchi hiyo kukopa

https://p.dw.com/p/127Aw
Rais Barack ObamaPicha: AP

Amesema kamati ya Congress itaundwa ili kuchunguza uwezekano wa kupunguza zaidi matumizi na kuongeza mapato ya kodi ambapo itatakiwa kutoa taarifa yake Novemba mwaka huu.

Hata hivyo mabaraza yote mawili, Congress na Seneti bado yatatakiwa kupiga kura kuuridhia mpango huo au la.Mpango huo ulikuwa akijadiliwa katika Ikulu ya Marekani na wanasiasa wa ngazi ya juu wa Demokrat na wale wa Republican.

Iwapo mpango huo utapitishwa, basi utamaliza wiki kadhaa za mvutano wa kisiasa.Marekani ina siku mbili tu hadi Jumanne usiku kufikia makubaliano ya kuongeza kiwango cha kuweza kukopa au ikabiliwe na hali ya kufilisika, jambo ambalo litakua na athari kubwa kwa uchumi wa dunia.