1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama akutana na Abbas na Netanyahu Washington

Josephat Nyiro Charo2 Septemba 2010

Juhudi mpya za kutafuta amani baina ya Israel na Wapalestina zagubikwa na mauaji ya Waisraeli wanne huko Ukingo wa Magharibi

https://p.dw.com/p/P2Dy
Rais wa Marekani, Barack Obama (katikati) waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanjahu (kushoto) na rais wa Wapalestina Mahmud AbbasPicha: picture-alliance/dpa

Rais wa Marekani Barack Obama amefanya mazungumzo na rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina, Mahmoud Abbas na waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu mjini Washington usiku wa kuamkia leo. Mkutano huo umefanyika kabla kuanza tena leo mazungumzo ya ana kwa ana kati ya pande hizo mbili katika kipindi cha karibu miaka miwili. Akizungumza na waandishi wa habari katika ikulu yake mjini Washington rais Obama amesema Marekani haitayumbishwa katika kuhakikisha usalama wa Israel.

Juhudi mpya za amani zimegubikwa na mauaji ya Waisraeli wanne na kundi la Hamas Jumanne usiku karibu na makaazi ya Wayahudi ya Kiryat Arba, katika eneo la Ukingo wa Magharibi. Kundi hilo limeapa kupinga juhudi za amani na kusema rais Abbas hana haki ya kufanya mashauriano kwa niaba ya Wapalestina.